Zaburi 77:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako. Neno: Bibilia Takatifu Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonesha uwezo wako kati ya mataifa. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa. BIBLIA KISWAHILI Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. |
Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.
Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila la watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lolote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.
Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.