Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Zaburi 77:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Biblia Habari Njema - BHND Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Neno: Bibilia Takatifu Nitayakumbuka matendo ya Mwenyezi Mungu; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. Neno: Maandiko Matakatifu Nitayakumbuka matendo ya bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. BIBLIA KISWAHILI Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. |
Isaka akatoka ili kutafakari shambani wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.
Maana hawazifahamu kazi za BWANA, Wala matendo ya mikono yake, Atawavunja wala hatawajenga tena;
Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu.
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.