Zaburi 76:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu aliposimama ili kuhukumu Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wakati ulipoinuka kutekeleza hukumu, kuwaokoa wote wanaodhulumiwa duniani. Biblia Habari Njema - BHND wakati ulipoinuka kutekeleza hukumu, kuwaokoa wote wanaodhulumiwa duniani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wakati ulipoinuka kutekeleza hukumu, kuwaokoa wote wanaodhulumiwa duniani. Neno: Bibilia Takatifu wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. Neno: Maandiko Matakatifu wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. BIBLIA KISWAHILI Mungu aliposimama ili kuhukumu Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia. |
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
BWANA akanena ghafla na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.
bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.