Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.
Zaburi 74:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Upite na kupaona palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pita juu ya magofu haya ya kudumu! Adui wameharibu kila kitu hekaluni. Biblia Habari Njema - BHND Pita juu ya magofu haya ya kudumu! Adui wameharibu kila kitu hekaluni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pita juu ya magofu haya ya kudumu! Adui wameharibu kila kitu hekaluni. Neno: Bibilia Takatifu Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. BIBLIA KISWAHILI Upite na kupaona palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu. |
Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kwenye kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?
Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.
Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu.
Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.
Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.
Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.
Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.
Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka.
Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.