Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Zaburi 73:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Udhalimu huwavika kama nguo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kiburi kimekuwa mkufu wao shingoni, uhasama ni kama nguo yao. Biblia Habari Njema - BHND Kiburi kimekuwa mkufu wao shingoni, uhasama ni kama nguo yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kiburi kimekuwa mkufu wao shingoni, uhasama ni kama nguo yao. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri. BIBLIA KISWAHILI Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Udhalimu huwavika kama nguo. |
Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimpandisha cheo Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akamwinua, akamwekea kiti chake juu ya wakuu wote waliokuwapo pamoja naye.
Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.
Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.
Umenishangaza moyo, dada yangu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Ujeuri wake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyojitukuza moyoni mwake.
Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Na uzani wa hizo herini za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia wao.