Hema za wanyang'anyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
Zaburi 73:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana niliwaonea wivu wenye kiburi, nilipoona wakosefu wakifanikiwa. Biblia Habari Njema - BHND maana niliwaonea wivu wenye kiburi, nilipoona wakosefu wakifanikiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana niliwaonea wivu wenye kiburi, nilipoona wakosefu wakifanikiwa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. BIBLIA KISWAHILI Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki. |
Hema za wanyang'anyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.
Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awakaripia.
Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.
Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?
Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?