Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
Zaburi 73:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama ningalisema hayo kama wao, ningalikuwa mhaini miongoni mwa watu wako. Biblia Habari Njema - BHND Kama ningalisema hayo kama wao, ningalikuwa mhaini miongoni mwa watu wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama ningalisema hayo kama wao, ningalikuwa mhaini miongoni mwa watu wako. Neno: Bibilia Takatifu Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningekuwa nimewasaliti watoto wako. Neno: Maandiko Matakatifu Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako. BIBLIA KISWAHILI Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako. |
Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
Bali ninyi mmegeuka mkaiacha njia; mmewakwaza watu wengi katika sheria; mmeliharibu agano la Lawi, asema BWANA wa majeshi.
Na ndugu yako akichukizwa kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa BWANA.