Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Zaburi 73:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivi ndivyo watu waovu walivyo; wana kila kitu na wanapata mali zaidi. Biblia Habari Njema - BHND Hivi ndivyo watu waovu walivyo; wana kila kitu na wanapata mali zaidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivi ndivyo watu waovu walivyo; wana kila kitu na wanapata mali zaidi. Neno: Bibilia Takatifu Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri. Neno: Maandiko Matakatifu Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri. BIBLIA KISWAHILI Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe siku zote wamepata mali nyingi. |
Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.