Zaburi 73:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanasema: “Mungu hawezi kujua! Mungu Mkuu hataweza kugundua!” Biblia Habari Njema - BHND Wanasema: “Mungu hawezi kujua! Mungu Mkuu hataweza kugundua!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanasema: “Mungu hawezi kujua! Mungu Mkuu hataweza kugundua!” Neno: Bibilia Takatifu Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” Neno: Maandiko Matakatifu Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” BIBLIA KISWAHILI Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu? |
Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;
Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.
Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.