BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Zaburi 72:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui zake wakaao nyikani wanyenyekee mbele yake, washindani wake walambe vumbi. Biblia Habari Njema - BHND Maadui zake wakaao nyikani wanyenyekee mbele yake, washindani wake walambe vumbi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui zake wakaao nyikani wanyenyekee mbele yake, washindani wake walambe vumbi. Neno: Bibilia Takatifu Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. Neno: Maandiko Matakatifu Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. BIBLIA KISWAHILI Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. |
BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.