Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Zaburi 71:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu; Biblia Habari Njema - BHND Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu; Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. BIBLIA KISWAHILI Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. |
Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akiwa bado mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa Maashera, na sanamu za kuchonga, na za kusubu.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, kama mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.
Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.