Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu Unijibu Kwa uaminifu wako, Unijibu kwa haki yako.
Zaburi 71:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa haki yako uniponye, uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa uadilifu wako uniokoe na kunisalimisha; unitegee sikio lako na kuniokoa! Biblia Habari Njema - BHND Kwa uadilifu wako uniokoe na kunisalimisha; unitegee sikio lako na kuniokoa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa uadilifu wako uniokoe na kunisalimisha; unitegee sikio lako na kuniokoa! Neno: Bibilia Takatifu Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. BIBLIA KISWAHILI Kwa haki yako uniponye, uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe. |
Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu Unijibu Kwa uaminifu wako, Unijibu kwa haki yako.
Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ngome thabiti ya kuniokoa.
Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.
Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.