Alimtumaini BWANA, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia.
Zaburi 71:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwako ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama; kamwe usiniache niaibike! Biblia Habari Njema - BHND Kwako ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama; kamwe usiniache niaibike! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwako ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama; kamwe usiniache niaibike! Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe. BIBLIA KISWAHILI Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. |
Alimtumaini BWANA, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia.
Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.
Bali Israeli wataokolewa na BWANA kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.
Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.