Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Zaburi 70:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!” Biblia Habari Njema - BHND Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!” Neno: Bibilia Takatifu Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “Mwenyezi Mungu ni mkuu!” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!” BIBLIA KISWAHILI Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. |
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Washangilie na wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, BWANA ni Mkuu.
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.