Zaburi 7:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uyakusanye mataifa kandokando yako, nawe uyatawale kutoka juu. Biblia Habari Njema - BHND Uyakusanye mataifa kandokando yako, nawe uyatawale kutoka juu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uyakusanye mataifa kandokando yako, nawe uyatawale kutoka juu. Neno: Bibilia Takatifu Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu. Neno: Maandiko Matakatifu Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu. BIBLIA KISWAHILI Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale. |
Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.
Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila.
Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.