Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Zaburi 7:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike. Biblia Habari Njema - BHND Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike. Neno: Bibilia Takatifu Amka kwa hasira yako, Ee Mwenyezi Mungu, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki. Neno: Maandiko Matakatifu Amka kwa hasira yako, Ee bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki. BIBLIA KISWAHILI BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu. |
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Nijapopitia katika shida, Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu, Unaunyosha mkono wako, Na mkono wako wa kulia unaniokoa.
Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.
BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila.
Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo;
Basi sasa, BWANA, Mungu wetu, utuokoe kutoka kwa mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.