Zaburi 7:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema basi, adui na anifuatie na kunikamata; ayakanyage maisha yangu; na kuniulia mbali. Biblia Habari Njema - BHND basi, adui na anifuatie na kunikamata; ayakanyage maisha yangu; na kuniulia mbali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza basi, adui na anifuatie na kunikamata; ayakanyage maisha yangu; na kuniulia mbali. Neno: Bibilia Takatifu basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini. Neno: Maandiko Matakatifu basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini. BIBLIA KISWAHILI Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini. |
Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, niliwakanyaga kwa hasira yangu, Niliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata.
Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.
Na sasa, angalia, ninajua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.