Nami mjakazi wako nilikuwa na wana wawili, na hao wawili wakashindana uwandani, wala hapakuwa na mtu wa kuwaamua, lakini mmoja akampiga mwenzake, akamwua.
Zaburi 7:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akaniburura hadi pasipokuwa na wa kuniponya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema La sivyo, watakuja kunirarua kama simba, wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa. Biblia Habari Njema - BHND La sivyo, watakuja kunirarua kama simba, wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza La sivyo, watakuja kunirarua kama simba, wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa. Neno: Bibilia Takatifu la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. Neno: Maandiko Matakatifu la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. BIBLIA KISWAHILI Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akaniburura hadi pasipokuwa na wa kuniponya. |
Nami mjakazi wako nilikuwa na wana wawili, na hao wawili wakashindana uwandani, wala hapakuwa na mtu wa kuwaamua, lakini mmoja akampiga mwenzake, akamwua.
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?
Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ngome thabiti ya kuniokoa.
Lakini nikijikwaa wanafurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wakanipapura bila kukoma.
Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Nilijituliza hata asubuhi; kama simba, anaivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Wala hakukuwa na mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa mbali sana na Sidoni, nao hawakutangamana na watu wowote wale; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo.