na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.
Zaburi 7:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema; nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema - BHND Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema; nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema; nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu. Neno: Bibilia Takatifu Nitamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana. Neno: Maandiko Matakatifu Nitamshukuru bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la bwana Aliye Juu Sana. BIBLIA KISWAHILI Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu. |
na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.
Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.
bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba huo mpango mwovu alioufanya juu ya Wayahudi umrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye Juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utanyeshewa na umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.
Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,
ili kwamba huo udhalimu waliotendewa hao wana sabini wa Yerubaali ulipizwe, ili damu yao iwe juu ya Abimeleki ndugu yao, aliyewaua, na juu ya watu wa Shekemu, waliomtia nguvu mikono yake ili awaue hao nduguze.
uovu wote wa watu wa Shekemu Mungu alilipiza juu ya vichwa vyao; na hiyo laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali ikawajia juu yao.