Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Zaburi 7:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake. Biblia Habari Njema - BHND Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atatayarisha silaha zake za hatari, na kuipasha moto mishale yake. Neno: Bibilia Takatifu Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. Neno: Maandiko Matakatifu Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. BIBLIA KISWAHILI Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto. |
Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto.
Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.
Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.
Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.
kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.
Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?