La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Zaburi 7:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu asipoongoka ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wasipoongoka, Mungu atanoa upanga wake; atavuta upinde wake na kulenga shabaha. Biblia Habari Njema - BHND Watu wasipoongoka, Mungu atanoa upanga wake; atavuta upinde wake na kulenga shabaha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wasipoongoka, Mungu atanoa upanga wake; atavuta upinde wake na kulenga shabaha. Neno: Bibilia Takatifu Mtu asipotubu, Mungu ataunoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. BIBLIA KISWAHILI Mtu asipoongoka ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari; |
La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni; tazama, utashukia Edomu, na juu ya watu wa laana yangu, ili kuwahukumu. Oba 1-14; Mal 1:2-5
Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.
Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.