Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Zaburi 7:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu ndiye ngao yangu; yeye huwaokoa wanyofu wa moyo. Biblia Habari Njema - BHND Mungu ndiye ngao yangu; yeye huwaokoa wanyofu wa moyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu ndiye ngao yangu; yeye huwaokoa wanyofu wa moyo. Neno: Bibilia Takatifu Ngao yangu ni Mungu Aliye Juu Sana, anayewaokoa wanyofu wa moyo. Neno: Maandiko Matakatifu Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo. BIBLIA KISWAHILI Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo. |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu);
Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye fikira na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.