Zaburi 69:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. BIBLIA KISWAHILI Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. |
Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
Basi Herode akamdhalilisha, pamoja na askari wake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.