Zaburi 69:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wazawa wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wazawa wa watumishi wake watairithi, wale wanaopenda jina lake wataishi humo. Biblia Habari Njema - BHND wazawa wa watumishi wake watairithi, wale wanaopenda jina lake wataishi humo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wazawa wa watumishi wake watairithi, wale wanaopenda jina lake wataishi humo. Neno: Bibilia Takatifu watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote wanaolipenda jina lake wataishi humo. Neno: Maandiko Matakatifu watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo. BIBLIA KISWAHILI Wazawa wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo. |
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;
Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA.
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.