Zaburi 69:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mungu atauokoa mji Siyoni, na kuijenga tena miji ya Yuda. Watu wake wataishi humo na kuimiliki; Biblia Habari Njema - BHND Maana Mungu atauokoa mji Siyoni, na kuijenga tena miji ya Yuda. Watu wake wataishi humo na kuimiliki; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Mungu atauokoa mji Siyoni, na kuijenga tena miji ya Yuda. Watu wake wataishi humo na kuimiliki; Neno: Bibilia Takatifu kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, BIBLIA KISWAHILI Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. |
Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;
Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.
Bali katika mlima Sayuni kutakuwa na watakaookoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki tena milki zao.
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.