Zaburi 69:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa. Neno: Maandiko Matakatifu bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Mungu huwapa wapweke makao yao; Huwapa wafungwa uhuru na kuwafanikisha; Bali wakaidi huishi katika nchi kavu.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.