Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonesha wokovu wa Mungu.
Zaburi 69:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jambo hili litampendeza Mwenyezi-Mungu zaidi, kuliko kumtolea tambiko ya ng'ombe, kuliko kumtolea fahali mzimamzima. Biblia Habari Njema - BHND Jambo hili litampendeza Mwenyezi-Mungu zaidi, kuliko kumtolea tambiko ya ng'ombe, kuliko kumtolea fahali mzimamzima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jambo hili litampendeza Mwenyezi-Mungu zaidi, kuliko kumtolea tambiko ya ng'ombe, kuliko kumtolea fahali mzimamzima. Neno: Bibilia Takatifu Hili litampendeza Mwenyezi Mungu kuliko ng’ombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. Neno: Maandiko Matakatifu Hili litampendeza bwana kuliko ng’ombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. BIBLIA KISWAHILI Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. |
Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonesha wokovu wa Mungu.
Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe.
Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.