Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani.
Kwa wimbo nitalisifu jina la Mungu, nitamtukuza kwa shukrani.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.