Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Zaburi 69:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niko hoi kwa kupiga yowe, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu. Biblia Habari Njema - BHND Niko hoi kwa kupiga yowe, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niko hoi kwa kupiga yowe, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu. Neno: Bibilia Takatifu Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. BIBLIA KISWAHILI Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo langu limekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu. |
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti
Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumainia BWANA.
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;