Zaburi 69:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, Mungu, wokovu wako utaniinua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mimi mnyonge na mgonjwa; uniinue juu, ee Mungu, uniokoe. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mimi mnyonge na mgonjwa; uniinue juu, ee Mungu, uniokoe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mimi mnyonge na mgonjwa; uniinue juu, ee Mungu, uniokoe. Neno: Bibilia Takatifu Lakini mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. Neno: Maandiko Matakatifu Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. BIBLIA KISWAHILI Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, Mungu, wokovu wako utaniinua. |
Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu mjeuri.
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie.
BWANA akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.