wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.
Zaburi 69:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uwaongezee uovu juu ya uovu, Wala wasipate msamaha kutoka kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwaadhibu kwa kila uovu wao; uwakatalie kabisa msamaha wako. Biblia Habari Njema - BHND Uwaadhibu kwa kila uovu wao; uwakatalie kabisa msamaha wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwaadhibu kwa kila uovu wao; uwakatalie kabisa msamaha wako. Neno: Bibilia Takatifu Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako. BIBLIA KISWAHILI Uwaongezee uovu juu ya uovu, Wala wasipate msamaha kutoka kwako. |
wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Farao akaufanya moyo wake kuwa mzito mara hiyo nayo, wala hakuwapa ruhusa hao watu waende zao.
BWANA akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyomwambia Musa.
Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa BWANA.
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao.
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
Iskanda, mfua shaba, alionesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa kulingana na matendo yake.