Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Zaburi 69:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Makambi yao na yawe ukiwa, Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kambi zao ziachwe mahame, asiishi yeyote katika mahema yao. Biblia Habari Njema - BHND Kambi zao ziachwe mahame, asiishi yeyote katika mahema yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kambi zao ziachwe mahame, asiishi yeyote katika mahema yao. Neno: Bibilia Takatifu Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. Neno: Maandiko Matakatifu Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. BIBLIA KISWAHILI Makambi yao na yawe ukiwa, Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao. |
Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu kuhusu shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;
Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hadi miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa;
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hadi mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine.