Zaburi 69:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe wajua ninavyotukanwa, wajua aibu na kashfa ninazopata; na maadui zangu wote wewe wawajua. Biblia Habari Njema - BHND Wewe wajua ninavyotukanwa, wajua aibu na kashfa ninazopata; na maadui zangu wote wewe wawajua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe wajua ninavyotukanwa, wajua aibu na kashfa ninazopata; na maadui zangu wote wewe wawajua. Neno: Bibilia Takatifu Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua. Neno: Maandiko Matakatifu Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua. BIBLIA KISWAHILI Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. |
Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.