Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.
Zaburi 69:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usimfiche mtumishi wako uso wako; unijibu haraka, maana niko hatarini. Biblia Habari Njema - BHND Usimfiche mtumishi wako uso wako; unijibu haraka, maana niko hatarini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usimfiche mtumishi wako uso wako; unijibu haraka, maana niko hatarini. Neno: Bibilia Takatifu Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. Neno: Maandiko Matakatifu Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. BIBLIA KISWAHILI Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi. |
Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.
Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Maana hapuuzi Wala kuchukizwa na mateso ya anayeteswa, Wala hamfichi uso wake, Bali humsikia akimlilia.
Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?