Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Zaburi 69:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu. Biblia Habari Njema - BHND Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. BIBLIA KISWAHILI Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. |
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nilijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
Ee BWANA, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki.
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.
Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.
Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.