basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.
Zaburi 69:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa kifani cha dharau kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau. Biblia Habari Njema - BHND Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau. Neno: Bibilia Takatifu Ninapovaa gunia, watu hunidharau. Neno: Maandiko Matakatifu Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau. BIBLIA KISWAHILI Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa kifani cha dharau kwao. |
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.
wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.
Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;
Naam, nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana, katika mahali pote nitakapowafukuzia.
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.