Zaburi 69:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniokoe, ee Mungu; maji yamenifika shingoni. Biblia Habari Njema - BHND Uniokoe, ee Mungu; maji yamenifika shingoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniokoe, ee Mungu; maji yamenifika shingoni. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. |
Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye Akuombe awapo katika dhiki. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maporomoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.
Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.