La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Zaburi 67:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana wawahukumu watu kwa haki, na kuyaongoza mataifa duniani. Biblia Habari Njema - BHND Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana wawahukumu watu kwa haki, na kuyaongoza mataifa duniani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana wawahukumu watu kwa haki, na kuyaongoza mataifa duniani. Neno: Bibilia Takatifu Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. Neno: Maandiko Matakatifu Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. BIBLIA KISWAHILI Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. |
La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.
Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu.
Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.
Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na uchungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.
Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.