Zaburi 67:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Njia yake ijulikane duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa. Biblia Habari Njema - BHND dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa. Neno: Bibilia Takatifu ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. Neno: Maandiko Matakatifu ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. BIBLIA KISWAHILI Njia yake ijulikane duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. |
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Maana nitamsifu tena, Aliye msaada wangu, Na Mungu wangu.
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.
Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.
Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa bidii habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu.
nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake.
Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.