Zaburi 67:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema; Biblia Habari Njema - BHND Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema; Neno: Bibilia Takatifu Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, Neno: Maandiko Matakatifu Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, BIBLIA KISWAHILI Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. |
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Uliniokoa nilipokuwa katika shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Ee BWANA, wasamehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao.