Zaburi 66:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai, Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye ametujalia maisha, wala hakutuacha tuanguke. Biblia Habari Njema - BHND Yeye ametujalia maisha, wala hakutuacha tuanguke. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye ametujalia maisha, wala hakutuacha tuanguke. Neno: Bibilia Takatifu ameyahifadhi maisha yetu na kuizuia miguu yetu kuteleza. Neno: Maandiko Matakatifu ameyahifadhi maisha yetu na kuizuia miguu yetu kuteleza. BIBLIA KISWAHILI Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai, Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe. |
Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazawa wake.
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya kombeo.