Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Zaburi 66:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Atawalaye kwa uweza wake milele; Ambaye macho yake yanaangalia mataifa; Hebu wanaoasi wasijitukuze nafsi zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anatawala milele kwa nguvu yake kuu; macho yake huchungulia mataifa yote. Mwasi yeyote asithubutu kumpinga. Biblia Habari Njema - BHND Anatawala milele kwa nguvu yake kuu; macho yake huchungulia mataifa yote. Mwasi yeyote asithubutu kumpinga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anatawala milele kwa nguvu yake kuu; macho yake huchungulia mataifa yote. Mwasi yeyote asithubutu kumpinga. Neno: Bibilia Takatifu Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote: waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote: waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. BIBLIA KISWAHILI Atawalaye kwa uweza wake milele; Ambaye macho yake yanaangalia mataifa; Hebu wanaoasi wasijitukuze nafsi zao. |
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Ufalme wako ni ufalme wa milele, BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote, Na mwenye fadhili katika matendo yake yote Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.
Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]