Zaburi 66:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Dunia yote inakuabudu; watu wote wanakuimbia sifa!” Biblia Habari Njema - BHND Dunia yote inakuabudu; watu wote wanakuimbia sifa!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Dunia yote inakuabudu; watu wote wanakuimbia sifa!” Neno: Bibilia Takatifu Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.” Neno: Maandiko Matakatifu Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.” BIBLIA KISWAHILI Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako. |
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Kwa mambo ya kutisha utatujibu, Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu. Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia, Na la bahari iliyo mbali sana,
Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.