Nilimwita kwa kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
Mimi nilimlilia msaada kwa sauti, sifa zake nikazitamka.
Nilimlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu.
Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.
Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
Ee BWANA, nilikulilia Wewe, Naam, kwa BWANA niliomba dua.
Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako?
Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.