Zaburi 66:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, Biblia Habari Njema - BHND Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, Neno: Bibilia Takatifu Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu: Neno: Maandiko Matakatifu Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu: BIBLIA KISWAHILI Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu; |
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
BWANA ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.
Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao.
Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA.
Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.
Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.
Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako.
Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.
Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.