Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 65:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Tutakapozidiwa na matendo maovu Wewe utatuondolea uovu wetu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tutakapozidiwa na matendo maovu Wewe utatuondolea uovu wetu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 65:3
21 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;


Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akisema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru, mimi nimekusikia.


Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.


Maana dhambi zangu zimenifunika kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno.


Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Nami nimevunjika moyo.


Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.


Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, utusamehe dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako.


akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.


Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.


Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.


Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi ya kuwatakasa kutoka kwa dhambi na kwa unajisi.


Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!


Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.


basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na dosari, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?


tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,