Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Zaburi 64:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wananoa ndimi zao kama upanga, wanafyatua maneno ya ukatili kama mishale. Biblia Habari Njema - BHND Wananoa ndimi zao kama upanga, wanafyatua maneno ya ukatili kama mishale. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wananoa ndimi zao kama upanga, wanafyatua maneno ya ukatili kama mishale. Neno: Bibilia Takatifu Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. Neno: Maandiko Matakatifu Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. BIBLIA KISWAHILI Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale, |
Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.