Zaburi 64:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Unifiche mbali na njama za watenda mabaya, Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unikinge na njama za waovu, na ghasia za watu wabaya. Biblia Habari Njema - BHND Unikinge na njama za waovu, na ghasia za watu wabaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unikinge na njama za waovu, na ghasia za watu wabaya. Neno: Bibilia Takatifu Unifiche kutokana na njama za waovu, kutokana na fitina za kundi la watenda maovu. Neno: Maandiko Matakatifu Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya. BIBLIA KISWAHILI Unifiche mbali na njama za watenda mabaya, Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu; |
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Maana atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.
Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.
Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.
Lakini wewe, BWANA, unajua mashauri yao yote juu yangu, ya kuniua; usiwasamehe uovu wao, wala usifute dhambi yao mbele za macho yako; bali wakwazwe mbele zako; uwatende mambo wakati wa hasira yako.
na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani.