Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.
Zaburi 60:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwape ishara wale wanaokuheshimu, wapate kuuepa mshale. Biblia Habari Njema - BHND Uwape ishara wale wanaokuheshimu, wapate kuuepa mshale. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwape ishara wale wanaokuheshimu, wapate kuuepa mshale. Neno: Bibilia Takatifu Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. BIBLIA KISWAHILI Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. |
Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.
Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli, upole na haki Na mkono wako wa kulia Utakutendea mambo ya ajabu.
Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.
Haya! Juu ya mlima usio na miti inueni bendera, wapazieni sauti zenu, wapungieni mkono, kwamba waingie katika malango ya wakuu.
Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.
Naye atawatolea ishara mataifa toka mbali, Naye atawapigia miruzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.
Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.