Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.
Zaburi 60:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, umetuacha kabisa, ee Mungu? Wewe huendi tena na majeshi yetu! Biblia Habari Njema - BHND Je, umetuacha kabisa, ee Mungu? Wewe huendi tena na majeshi yetu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, umetuacha kabisa, ee Mungu? Wewe huendi tena na majeshi yetu! Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? |
Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.
Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
BWANA akaniambia, Waambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi siko kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu.
kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,
Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.